Events
Photos and videos from events held during COP12, published by the secretariat.
Rasilimali za bahari zinapaswa kulindwa ili ziweze kuhifadhi mazingira ya bahari na kuwanufaisha wananchi kiuchumi
Tulinde bahari na rasilimali zake tukuze uchumi wetu
Video hii inalenga kuhamasisha ushiriki na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa COP12 na fursa inayotolewa na Tanzania kuwa mwenyeji wa tukio hili muhimu la kimataifa.
Tanzania inajivunia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 6 hadi 9 Oktoba 2026. Mkutano huu wa kimataifa unaoadhimisha miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi utawakutanisha wadau kutoka nchi za Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi kujadili ulinzi na uhifadhi wa mazingira ya bahari na pwani, mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai na maendeleo ya Uchumi wa Buluu Endelevu kwa manufaa ya watu na mazingira.

Kutoka baharını hadi Jukwaa la Dunia, ni COP12 hapa Tanzania