Nairobi ConventionCOP12 Tanzania 2026
5 September 2026

COP12 Tanzania

Tanzania inajivunia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 6 hadi 9 Oktoba 2026. Mkutano huu wa kimataifa unaoadhimisha miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi utawakutanisha wadau kutoka nchi za Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi kujadili ulinzi na uhifadhi wa mazingira ya bahari na pwani, mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai na maendeleo ya Uchumi wa Buluu Endelevu kwa manufaa ya watu na mazingira.